TIRA NA NHIF ZASISITIZA ELIMU YA BIMA KWA WANANCHI

 

 Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) zimesisitiza umuhimu wa elimu kwa umma kuhusu bima ili kuongeza uelewa na matumizi ya huduma hizo nchini.

Msisitizo huo umetolewa wakati wa Kongamano la Wadau wa Habari, Waandishi wa Habari na Wahariri lililofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Mwanza.

Akizungumza katika kongamano hilo, mwakilishi wa TIRA, Khalifan amesema moja ya majukumu ya mamlaka hiyo ni kuhakikisha wananchi wanapata elimu sahihi kuhusu masuala ya bima.

Kwa upande wake, mwakilishi wa NHIF, Dkt. Julieth Muhanika(Afisa Udhibiti ubora)  amesema mfuko huo unaendelea kuboresha huduma zake, ikiwemo fao la Umoja Afya lenye mchango wa shilingi 60,000 kwa mwaka, pamoja na mfumo wa NHIF kiganjani unaowawezesha wanachama kufuatilia michango yao kwa urahisi.

Afisa udhibiti ubora na mahusiano kutoka NHIF Dkt. Julieth Muhanika

Amesema kifurushi cha Bima ya Afya kwa wote kinajumuisha huduma 372, zikiwemo huduma za daktari, kulazwa hospitalini, vipimo, dawa na upasuaji mkubwa na mdogo.

Aidha, takwimu zilizowasilishwa zinaonesha kuwa hadi Juni 2026, wazee 196 kati ya 235 waliotambuliwa walikuwa wamepatiwa kadi za bima ya afya sawa na asilimia 83 ya lengo lililowekwa.

Hata hivyo, NHIF imeeleza kuwa imani potofu kuhusu bima ya afya bado ni changamoto, hivyo kuendelea kutolewa kwa elimu kwa umma ni muhimu katika kuongeza uelewa wa wananchi na kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za afya.







Previous Post Next Post