Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Stadi (VETA) imeanzisha mradi wa mafunzo kuhusu shughuli za uchimbaji wa
madini kwa kutumia mitaala mipya sita, ikiwa ni hatua ya kukuza ujuzi na
matumizi ya teknolojia katika sekta ya madini nchini.
Meneja wa Uhusiano na Masoko,
Sita Peter amesema mradi huo utagusa maeneo mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Geita
ambao una mchango mkubwa katika sekta ya madini. Amesema VETA imeendelea kutoa
mafunzo mbalimbali yanayohusiana na teknolijia ya uchimbaji wa madini, huku ikilenga
kuwajengea wananchi na wadau ujuzi unaoendana na mahitaji ya sekta hiyo.
“Mradi wa madini muhimu
ambao unafadhiliwa na European Union, katika mradi huu tunakwenda kuanzisha
mafunzo kwenye maeneo mbalimbali ambayo
yanafanya shughuli za uchimbaji wa madini, na miongoni mwa maeneo ni Geita” aliseme
Sita Peter
Kauli hiyo imetolewa wakati wa Maonyesho ya tisa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika mkoani Geita yakilenga kuonyesha fursa, ubunifu na teknolojia zinazoweza kuimarisha ujuzi na tija katika shughuli za uchimbaji wa madini.
PICHA ZAIDI