WAKULIMA WATAKIWA KUZINGATIA USAFI NA UBORA WA PAMBA


Wakulima wa pamba wametakiwa kuzingatia usafi wakati wa kuvuna, kuhifadhi na kusafirisha zao hilo ili kuongeza ubora na ushindani wa pamba ya Tanzania katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

Afisa Kilimo kutoka Bodi ya Pamba, Doto Ntumba, amesema Tanzania ina maabara ya usanifu wa pamba iliyopo Shinyanga inayohudumia pia nchi za Kenya na Uganda, huku ikiwa na vitengo vya usanifu wa pamba kwa mikono na kwa kutumia mashine.

"Hapa tuna maabara za aina mbili, maabara ya usanifu wa mikono na maabara ya usanifu wa mashine.Wataalamu wetu wanapokea sampuli na kutoa madaraja ya pamba.Wakulima wakielimika, nasi tutaweza kuwa na pamba safi na tutauza kwenye soko, na pamba yetu itanunuliwa kwa wingi sana" amesema Doto

Amesema baadhi ya wakulima bado huchanganya pamba na uchafu wakati wa uvunaji, uhifadhi na usafirishaji, jambo linaloweza kushusha daraja na thamani ya zao hilo sokoni.

Doto amewataka waandishi wa habari kuongeza elimu kwa wakulima kuhusu mbinu bora za kushughulikia pamba, akisisitiza kuwa pamba safi na yenye ubora inaweza kuongeza mahitaji na soko la zao hilo.

Wakati huohuo, maandalizi yamefanyika kwa ajili ya kuanzishwa kwa ekari 1,000 za kongani za viwanda katika eneo la Misungwi, hatua inayolenga kuongeza thamani ya pamba na kuchochea uchakataji pamoja na shughuli za viwand
Previous Post Next Post