KADAMA ENGLISH MEDIUM YAONGOZA KANDA YA ZIWA MTIHANI WA TAPIE



 Kadama English Medium imeshika nafasi ya kwanza katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba wa Kanda ya Ziwa ulioandaliwa na Umoja wa Wamiliki wa Shule Binafsi Kanda ya Ziwa kupitia Tanzania Association of Private Investors in Education (TAPIE).

 

Katika matokeo hayo Kadama English Medium imepata wastani wa alama 47.7 ambao ni ambalo ni  daraja A huku wanafunzi wote wa shule hiyo waliofanya mtihani wamefanikiwa kupata wastani wa Daraja A.

 

Ushindi huo umeifanya shule hiyo kushika nafasi ya kwanza kati ya shule 17 zilizoshiriki katika mtihani huo wa pamoja wa Kanda ya Ziwa.  Mkurugenzi wa Kadama English Medium Leticia Pastory amesema shule hiyo itaendelea kuweka mkazo katika kuhakikisha inatoa elimu bora pamoja na maandalizi mazuri ya wanafunzi kwa ajili ya mitihani ya kitaifa.

 

Aidha amewataka wazazi kuendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa shule hiyo ili iweze kuendeleza tunu yake ya kuwapatia wanafunzi elimu bora pamoja na malezi yanayozingatia maadili mema.

 

Previous Post Next Post